Health & Fitness

Health & Fitness

For the love of Green Tea | Health and Fitness

August 5, 2017
greentea

Hey loves… so, it is weekend, Yay! 🙂 Who doesn’t like weekends? I love weekends, not because I wouldn’t be working, I will be, but it will be more fun, it’s weekend, working from home, with less fancy clothes, hello!

Did I ever mention that I am not a coffee person? Yes, now you know. I was a big fan of coffee, six months ago or so! The smell of it was so refreshing, I still find it refreshing I just don’t drink it anymore!

So, that being said I am happy to officially announce that I am a tea person, a dedicated one if you may. There is something about tea (chai in Swahili) that I like, it so calming, refreshing and healthy at the same time.

I have been drinking black tea since I was very you, my mother is a tea person from the heart so tea was always available in the kitchen.

After going to college and staying on my own I switched from black tea to coffee, well the busy life of college comes with the need for some caffeine in coffee to keep you going.

After college, I changed my life to healthy eating and fitness then I switched back to tea but this time it wasn’t black tea, it was herbal teas, specifically green tea or hibiscus tea with no sugar.

These have been my go to and I have never looked back. And here is why I love green tea which I drink at least two cups every day: you can read about why hibiscus tea is good for you here.

Why green tea is my go to;

green tea

I do it for the fun of it

Drinking tea is fun, drinking anything is fun 🙂 unless that something will make you go crazy and lose your mind or waking up with a hell of a hangover.

For me when I drink my tea I get some thinking going on in my mind, I make some of my important decisions or not so important decision when I have a cup in my hand. It is refreshing and makes me focus for some time and I like that.

I do it for my skin

So, I love my skin. Even though I have been having some issues with it recently but I still love it. With all these issues I have had green has been there to help as I mentioned I drink at least two cups every day. Green tea help with inflammatory, acne and reduces wrinkles and it is anti-bacterial.

So if you have some issues with your skin you should definitely try switching to green tea. It takes some time to show results but I assure you, it helps.

Shed some weight

If you are looking to shed some weight away, then green tea should be your go to drink. I have been drinking green tea for a long time now, even though I switch to hibiscus sometime I can say I have managed to stay at the same weight for quite some time now. I exercise at least 3 times a week but still, I think green tea helps as well.

Green tea can prevent cancer

Green tea is said to be helpful in preventing quite a number of cancer types. Cancer is no joke if a few cups of green tea can help prevent this monster why not dedicate yourself to drinking it at least a cup or two every day? Besides it is no hard work, it is tea, hello!

Cancers like that of skin, lung, ovarian, breast, stomach and prostate can be prevented by green tea. This gives me more reasons to love green tea every day.

This is not a guarantee that you can prevent it 100% but even if it’s only 1% wouldn’t you give it a go? You have nothing to lose!

I do It for my heart

green tea and heart

I love the sound of my heart beat whenever I get up in the morning, I know it is another day of life, another chance to keep on living! Do you know how much work your heart is doing to make sure you wake up in the morning? Before you continue reading this, show some respect and say thank you for the hard work.

To show that you mean what you just said get yourself a few cups of green tea today as a gratitude token for your heart.

It is said that people who drink at least 5 cups of green tea every day have a significantly lower risk of dying of heart diseases than those who drink less than one cup a day.

So, you still don’t want to drink a cup of green tea at least once a day? Come on, it is the least you can do for your body considering everything that is doing for you.
What is your go to herbal tea? Leave a comment below.

Reference:here

Until our next talk,

JS 🙂

Health & Fitness

Ujali mwili wako, ni sehemu pekee unayoishi | Health

July 5, 2017
maji - Ujali mwili wako, ni sehemu pekee unayoishi | Health

Jana nimekaa nyumbani nikajiuliza ni kiasi gani mwili wangu unanihitaji na ni kwa kiasi gani nina uhitaji mwili wangu?

Nikagundua ninauhitaji mwili wangu zaidi ya vile ambavyo unanihitaji mimi kwasababu mimi ninaishi ndani yake.

Licha tu ya kuishi ndani yake, mwili wangu ni sehemu pekee ambayo nitaishi kwa muda wote nitakaokaa hapa duniani hivyo basi sina budi kuujali na kuutunza kwa vyovyote vile niwezevyo kwani kama mwili wangu hautakuwa na afya njema basi sitaweza kufikia ndoto nilizojiwekea katika maisha yangu.

Kama mwili wangu hautakuwa na afya njema sitaweza kuwapenda na kuwajali watu nianaowapenda kwani itanibidi nitumie muda huo kuuuguza mwili wangu.

Wala sitaweza kufurahia maisha yangu hapa duniani wala kufurahia mafanikio yoyote nitakayoyapata.

Haya hapa ni mambo kadhaa ambayo nimeamua kuyafanya ili afya ya mwili wangu iendelee kuwa bora na niendelee kufurahia zawadi ya uhai tuliyopewa na Mungu;

1. Kuwa makini na chakula Kinachoingia mwilini

afya ya mwili

Afya bora hujengwa na vyakula vyenye virutubisho na madini muhimu kwa mwili wa binadamu. Ili kuweza kupata virubisho na madini haya muhimu ni lazima upate mlo kamili ambao unajumuishwa na madini mbalimbali, vitamin mbalimbali, matunda, mboga za majani, vyakula vyenye protini na wanga.

Hakikisha unakuwa muangalifu na matumizi yako ya sukari, mafuta na chumvi. Aina hii ya vyakula inapozidi mwilini huweza kusababisha matatizo mbalimbali kama vile kisukari, magonjwa ya moyo na kuongezeka uzito uliokithiri ambao baadae utakuletea matatizo.

Unapopata chakula chako cha wanga hakikisha unapata wanga ambayo haijakoborewa.

Kwa mfano badala ya kula unga wa sembe jaribu kutafuta dona ili uweze kupata virutubisho vingi zaidi. Vivyo hivyo unapotaka kupika kitu kwa unga wa ngano basi chukua ngano ambayo haijakoborewa.

mimba

Hakikisha unaosha mboga za majani na matunda kabla ya matumizi yoyote na pia osha mikono yako kabla ya kuandaa chakula. Hakikisha unazingatia usafi wa chakula chako.

2. Fanya mazoezi

mazoezi - Ujali mwili wako, ni sehemu pekee unayoishi | Health

Ili kuweka mwili wako kuwa wenye nguvu na wenye afya bora ni lazima ufanye mazoezi ya viungo. Kufanya mazoezi kuna faida nyingi sana kwa afya yako.

Mazoezi husaidia kuimarisha misuli na mishipa, husaidia kuboresha usingizi wako, mazoezi pia husaidia kuufanya mwili wako kuwa na uzito sahihi na hivyo kukuepusha na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya moyo.

Aina ya mazoezi ya viungo hutegemea zaidi na mwili wako na umri wako, si kila mazoezi yanaweza kukufaa hivyo inashauriwa kumwona daktari au mtaalamu wa mazoezi ili kupata ushauri wa mazoezi yaliyo sahihi kwako.

3. Kunywa maji ya kutosha

maji - Ujali mwili wako, ni sehemu pekee unayoishi | Health

Maji yana umuhimu mkubwa sana katika mwili wa binadamu. Inasemekana kuwa mwili wa binadamu umeundwa na maji kwa zaidi ya asilimia 75.

Mwili hupoteza lita 2 hadi tatu kwa siku katika shughuli mbalimbali za mwili kwa mfano kukojoa, kutoka jasho, kupumua na kiwango hiki huongezeka zaidi pale unapokuwa mgonjwa, unaponyonyesha, unapokuwa mjazito au unapofanya mazoezi makali na kufanya kazi ngumu.

Kiwango hiki cha maji kinachopotea huweza kurudishwa kwa kunywa maji safi na salama na si kwa njia nyingine.

Dalili za kutokunywa maji ya kutosha huonekana katika midomo yako (pale unapokuwa mkavu), kukojoa mkojo wa njano iliyokolea, kutopata choo au kupata choo kigumu, magonjwa katika njia ya mkojo na kuongezeka uzito.

Hakikisha unakunywa maji zaidi ya lita 2 mpaka tatu kwa siku (kulingana na uzito wako). Usisubiri kunywa maji mpaka pale unaposikia kiu tu, kuwa na utaratibu wa kunywa maji angalau glasi moja baada ya masaa mawili.

Kwa taarifa zaidi za taratibu za kunywa maji soma hapa Fadhili.com

4. Usivute Sigara

Uvutaji wa sigara una madhara mengi ya kiafya katika mwili wako ingawa madhara hayo hayaonekani kwa muda mfupi lakini madhara yake ni makubwa sana, sigara ina kemikali ya nicotine ambayo huufikia ubongo wa mvutaji kwa sekunde saba mpaka kumi.

Baada ya moshi wa sigara kuvutwa na kemikali hiyo husambaa katika sehemu mbalimbali za mwili na hata kufikia katika maziwa ya mama ambapo basi kama mama ananyonyesha sumu hiyo huenda moja kwa moja kwa mtoto.

uvutaji wa sigara - Ujali mwili wako, ni sehemu pekee unayoishi | Health

Uvutaji wa sigara husababisha kansa ya mapafu, magonjwa ya moyo, na matatizo katika mfumo wa upumuaji.

Kwahiyo usipo vuta sigara utajiweka katika hali nzuri ya afya yako huku ukiendelea kutimiza malengo yako katika maisha, kama wewe ni mvutaji wa sigara itakuwa vizuri kama utachukua uamuzi wa kuacha ili kuilinda afya yako.

5. Pata usingizi wa kutosha

Akili na mwili wa binadamu huchoshwa na shughuli zinazofanyika kila siku hivyo basi usingizi wa kutosha ni muhimu sana kwa afya bora ya mwili wako.

Kiwango cha usingizi unaotakiwa kwa afya yako huzingatia umri wa mtu kwa mfano mtoto mchanga anahitaji usingizi wa masaa 16 mpaka 18 kwa siku, wakati mtu mzima anahitaji usingizi wa masaa 7 mpaka 8.

sleeping - Ujali mwili wako, ni sehemu pekee unayoishi | Health

Usingizi husaidia kupumzisha akili na mwili wako na kujiandaa kwa siku mpya. Husaidia kukufanya ujisikie mwenye nguvu na mwenye furaha zaidi kwani husaidia kupunguza msongo wa mawazo.

Usingizi mzuri pia husaidia ukuaji sahihi wa watoto, husaidia kurekebisha homoni mwilini na kudhibiti uzito sahihi wa mwili.

Njia nzuri ya kuboresha usingizi wako ni kulala na kuamka muda ule ule kila siku, hii itasaidia ubongo wako kukuandaa pale unapotaka kulala na unapotaka kuamka. Pia jizuie kula chakula kingi wakati wa usiku au kunywa kahawa baada ya saa kumi jioni.

Kuwa na afya bora kunahitaji umakini mkubwa sana. Hayo ni baadhi tu ya mambo ya msingi unayoweza kuyafanya ili kuweza kuiweka afya yako katika ubora zaidi.

Kumbuka afya bora ni mwanzo wa kutimiza ndoto za maisha yako, tunza afya yako.

Health & Fitness

Maambukizi Katika Mfumo Wa Mkojo (U.T.I) | Health

June 28, 2017
mkojo

Maambukizi katika mfumo wa mkojo ni maambukizi ambayo yanaathiri viungo vya mfumo wa mkojo. Mara nyingi watu wamezoea kusema U.T.I ambayo ni kifupisho cha Urinary Tract Infection.

Viungo hivyo hujumuisha figo, mirija inayopitisha mkojo kutoka kwenye figo hadi kwenye kibofu (ureta), kibofu na mrija wa kutolea mkojo nje ya mwili (urethra).

Maambukizi haya yamekua yakiwasumbua watu wengi wa jinsia zote. Wanawake ndio wamekuwa wakisumbuliwa zaidi na tatizo hili kutokana na maumbile yao. Watoto pia wanaweza kuathiriwa na tatizo hili hasa wale wa kike chini ya umri wa miaka miwili na mara nyingi dalili zake kwa watoto huwa si wazi.

Asilimia kubwa tatizo hili husababishwa na vimelea vya Escherichia coli (E. Coli), vimelea hawa kwa kawaida huishi katika utumbo wa binadamu bila kusababisha mdhara yoyote ila wapohamishwa kwenda sehemu nyingine huleta madhara (normal frola).

Vimelea hawa hufika kwenye mirija ya kutolea mkojo pale ambapo muhusika anashindwa kujisafisha vizuri baada yakujisaidia haja kubwa kwani hutolewa nje ya mwili pamoja na haja kubwa, vilevile kwa njia ya kujamiaana. Pia kuna aina nyingine za vimelea ambazo husababisha tatizo hili ukiacha na E.Coli. vimelea hawa husambaa kelekea kwenye kibofu na wakati mwingine hufika kwenye figo ikiwa mgonjwa hatatibiwa mapema.

Wanawake wanaathiriwa zaidi na tatizo hili kwa sababu wana mrija mfupi wa kutolea mkojo pia ukaribu uliopo kati ya sehemu ya kutolea haja kubwa na mrija wa kutolea mkojo. Pia wanawake wanaojamiiana maranyingi wako katika hatari ya kupata tatizo hilo.

Sababu nyingine ni kama kupungukiwa kinga mwilini, wagonjwa wliowekewa mirija ya kukojelea kwa muda mrefu(catheter),vile vile kuziba kwa njia ya mkojo.
Aina za U.T.I

zimegawanyanyika kutokana na kiungo kinachokuwa kimeathirika. Kwenye figo ambapo kwa jina la kitaalam inaitwa pylonephritis, kwenye kibofu inafahamika kama cystitis na kwenye urethra inafahamika kama urethritis.

Dalili za UTI ni pamoja na:

-kukojoa mara kwa mara na wakati mwingine kupata mkojo kidogo,
-maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo ambayo yanakua kama yanaunguza( burning sensation),
-maumivu ya kichwa pamoja na homa,
-kukojoa mkojo wenye harufu kali pia unaweza kuwa umechanganyikana na damu au unakua na ukungu Fulani,
-maumivu ya tumbo chini ya kitovu.
-Wakati mwingine mwili kukosa nguvu pia kukosa hamu ya kula.

Ni vizuri kufanya vipimo kabla ya kuanza kutumia dawa mara nyingi kipimo kinachotumika ni kuupima mkojo wa mgonjwa (urine analysis)

Maambukizi ya mfumo wa mkojo yanatibika kutumia dawa aina antibayotiki ambazo mgonjwa ana takiwa anywe dozi iliyokamilika na kwa usahihi. Tiba hii hutegemeana na umri, ujauzito na kuwepo kwa hali zingine. Pia huzingatia na usambaji wa vimelea yaani UTI kali na isiyo kali.

UTI isipotibiwa inaweza kusababisha madhara makubwa kama kuharibika kwa figo, kwa wajawazito wanaweza kujifungua watoto wenye uzito pungufu vile vile mirija ya mkojo kupungua sababu ya makovu.
Jinsi ya kujikinginga na maambukizi katika njia ya mkojo, mwanamke inatakiwa ajifunze jinsi ya kujisafisha baada ya kujisaidia haja kubwa; badala ya kujisafifisha kutoka nyuma kwenda mbele inatakiwa aanze mbele na amalizie nyuma ili kuepusha kinyesi kufika katika njia ya mkojo.

Pia kunywa maji mengi husaidia mtu kupata haja ndogo mara kwa mara hivyo kupunguza idadi ya vimelea katika njia ya mkojo na hivyo kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi katika njia ya mkojo.

Kutokukaa na mkojo kwa muda mrefu, hakikisha kila unaposikia haja ndogo hakikisha unaenda kujisaidia. Pia kubadili nguo za ndani mara kwa mara kwa wanawake husaidia na sisiwe zinabana sana. Bila kusahau kusafisha vyoo kabla na baada ya kujisaidia.

pineaple - Maambukizi Katika Mfumo Wa Mkojo (U.T.I) | Health

Matunda yanayoweza kusaidia UTI:

-Juice ya Malimao
-Juice ya machungwa
-Mananasi
-Epo
-Vitunguu saumu
-Tangawizi

Health & Fitness

Mambo Ya Kuzingatia Kabla Ya Kushika Mimba

June 22, 2017
Pregnancy, mimba, health

By Julie Evarist

Katika mazingira yetu tunayoishi hasa nchi zinazoendelea kama Tanzania ni watu wachache ambao huwa wanazingatia na kupanga mikakati ya afya zao kabla ya kushika ujauzito. Wengi wetu huwa hatufanyi maaandalizi ya kutosha na hivyo kusababisha matatizo kipindi cha ujauzito na wengine kushindwa kabisa kushika ujauzito .

Kabla ya hayo kuongea na mwenza wako ni jambo la muhimu ili kukubaliana kama wote wawili mpo tayari kwa jambo hilo, hii pia husaidia kupata msaada hasa kwa mama kipindi cha ujauzito.

Haya ni mambo machache ya muhimu ambayo yanatakiwa kuzingatiwa kabla mtu hajashika ujauzito:

1. Kupima afya yako na muenza wako.

kupima afya kabla ya ujauzito ni jambo la muhimu kwa sababu kuna baadhi ya magonjwa humuaathiri mtoto anapokua tumboni au wakati wa kuzaliwa.vipimo ambavyo ni muhimu ni kile cha virusi vya ukimwi ambapo kama mama ana maambukizi anaweza kumuambukiza mtoto. Pia kupiuma na kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya zinaa ni muhimu kwani yanaweza kusababisha mimba kutoka, mtoto kuzaliwa na maambukizi pia.

2. Kupata chanjo muhimu

Kuna chanjo muhimu ambazo humsaidia mama pia na mtoto. Moja ya chanjo hizo ambayo muhimu ni tetenasi ambayo katika mazingira yetu mama mjamzito huanza kuchoma sindano pale anapohudhuria kliniki kwa mara kwanza anapokua mjamzito. Siyo vibaya ukaanza sindando hizi kabla ya ujauzito ili mwili uanze kutengeneza kinga mapema. Sindano hizi huwa ni tano na zinapatika katika hospitali na huchomwa kwa ratiba hivi ni vizuri ukazingatia ratiba hiyo.

3. Acha matumizi ya njia za uzazi wa mpango

Kwa Yule ambae anatumia njia za uzazi wa mpango kama vidonge, sindano, vipandikizi na vijiti ina takiwa kuacha miezi kadhaa kabla ya kutaka kushika ujauzito. Hii itakusaidia kujua mzunguko wa siku zako za hedhi(mzuko wa asili) vizuri na kujua ni siku zipi zina uwezakano mkubwa wa kupata mimba.
Anza kutumia virutubisho mapema

Virutubisho ambavyo ni muhimu ni kama folic acid ambazo hujijenga katika mwili taratibu hivyo ni vema mtu ukaanza kuzitumia mapema (miezi mitatu kabla ya ujauzito) ili mda unapofika zinakua zimejijenga za kutosha katika mwili. Folic acid inapopungua mwilini kipindi cha ujauzito inaweza kusababisha mtoto akazaliwa na hali inayofahamika kama neural tube defect (spinal bifida) Pia ni vema ukapata vyakula vyenye vitamin mbalimbali kwani husaidia katika kupata ujauzito.

Kwa wale ambao wanatumia sigara na vinywaji nyenye kilevi ni vizuri ukaacha kabla ya ujauzito kwani vina madhara katika kupata ujauzito na kipindi cha ujauzito pia. Na hii si kwa mwanamke tuu, unywaji wa pombe kupindukia unaweza kupunguza uwezo wa mwanaume kuzalisha mbegu ambazo hazina uwezo wa kusababisha mimba.

Pia kabla ya kushika mimba mama anatakiwa kuacha matumizi ya vinywaji vyenye kafeini kama soda ambazo zina caffeine, kahawa na chai ya majani mengi kwani ni si vizuri kipindi cha ujauzito. Hivyo kuacha mapema itakusaidia usipate shida kipindi cha ujauzito.

4. kupunguza msongo wa mawazo

Pia ni vizuri pale unapojiiandaa kushika mimba kwani inaweza kuaharibu mzunguko wa siku kwa wanawake.

Mazoezi pia ni jambo la muhimu ili kupunguza uzito kwa wale wenye kilo zinazozidi wanasayansi wanahususianisha uwezo wa kupata mimba na uzito. Mwanamke mwenye uzito wa kati anauwezo mkubwa wa kupata mimba kuliko wenye uzito mkubwa.

mimba

Vyakula vyenye folic asid na vitamin ni pamoja na:

1. Mboga za majani (spinachi, figiri, brokoli, kabichi,
2. Citrus fruits (Machngwa, machenza, papai)
3. Maharage (aina zote)
4. Wali
5. Mkate (brown bread)
6. Parachichi
7. Mbegu za mimea (karanga, alizeti,)
8. Mahindi mabichi (kuchoma au kuchemsha)
9. Karoti
10. Viazi vitamu